Mark 8:20-30

20 a “Je, nilipoimega ile mikate saba kuwalisha watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?”

Wakamjibu, “Saba.”

21 bNdipo akawauliza, “Je, bado hamwelewi?”

Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida

22 cWakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Yesu amguse. 23 dYesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamuuliza, “Unaona chochote?”

24Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea.”

25Yesu akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. 26 eYesu akamuaga aende nyumbani kwake, akimwambia, “Hata kijijini usiingie.”

Petro Amkiri Yesu Kuwa Ndiye Kristo

(Mathayo 16:13-20; Luka 9:18-21)

27 fYesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

28 gWakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya, na bado wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”

29 hAkawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo.”
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.


30 jYesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake.

Copyright information for SwhNEN